Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika mafundisho ya dini, kipindi kabla ya kudhihiri Imam Mahdi (aj) kimeelezewa kama zama ambazo dunia itajaa dhulma na uonevu, wazo hili limekokotezwa katika hadithi nyingi, ikiwemo hadithi mashuhuri ya Mtume Mtukufu (saw) isemayo:
«یملأ الأرض قسطًا وعدلًا کما ملئت ظلمًا وجورًا»
"Ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama ilivyojazwa kwa dhulma na uonevu."
(Bihar al-Anwar, Juz. 52, uk. 340)
Hata hivyo, swali linazuka:
“Tunawezaje kuelewa uhusiano kati ya kujaa dunia kwa dhulma na kudhihiri Imam Mahdi (aj)? Je, kuenea kwa dhulma ni kisababisho cha kuharakisha kudhihiri au ni hali tu ambayo ndani yake dhuhuri inatimia?”
“Je, hili linamaanisha kwamba tunapaswa kunyamazia uonevu ili kuandaa mazingira ya kudhihiri? Je, mtazamo huu unaweza kutupotosha kutoka katika majukumu ya kijamii na kupambana na ukosefu wa haki?”
Kwa kuchunguza mada hii, swali liliulizwa kwa Hujjatul Islam Reza Parchabaf, mtaalamu wa masuala ya kimaadili, ambaye kwa kurejelea Aya, hadithi na mitazamo ya wanazuoni wakubwa, alieleza uhusiano kati ya dhulma na kudhihiri, yafuatayo ni maelezo kamili ya maelezo hayo:
بسم الله الرحمن الرحیم
Dhulma ni sharti linaloandaa mazingira ya kudhihiri, siyo sababu ya moja kwa moja, katika hadithi mashuhuri ya Mtume (saw):
«یملأ الأرض قسطًا وعدلًا کما ملئت ظلمًا وجورًا»
"Ataijaza dunia kwa uadilifu na haki kama ilivyojazwa kwa dhulma na uonevu."
(Bihar al-Anwar, Juz. 52, uk. 340)
Allamah Tabataba’i amesema: Kujazwa dunia kwa dhulma kunadhihirisha kuandaliwa kwa mazingira muhimu ya kudhihiri, na si kwamba dhulma ndiyo inayo sababisha kudhihiri.
(al-Mizan, Juz. 12, uk. 327).
Tunapaswa kutofautisha kati ya wajibu wa mtu binafsi na wajibu wa kijamii, katika nyanja ya mtu binafsi wakati wa ghaiba, amr bil ma’ruf na nahi anil munkar (Aali Imran:110) ni jambo lalazima, katika nyanja ya kijamii wakati wa ghaiba, kuunda mfumo wa haki kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kudhihiri itakuwa wajibu, mfano ni mapinduzi ya Imam Husayn (as) dhidi ya dhulma, ambayo ni kielelezo cha kupambana kabla ya kudhihiri.
Shahidi Murtadha Mutahhari alieleza nadharia ya “kusubiri kwa njia hai” pale aliposema: "Kusubiri kunamaanisha kuandaa mazingira ya kudhihiri kupitia kupambana na dhulma."
(Qiyam wa Inquilab-e Mahdi, uk. 25).
Kwa hiyo, shughuli za kijamii kama vile kudai uadilifu, mafunzo ya kimaadili na kupambana na ufisadi, ni vielelezo vya kusubiri.
Kwa mujibu wa kanuni ya «نفی سبیل» (an-Nisa:141): Kuhifadhi uhuru wa jamii ya Kiislamu dhidi ya utawala wa madhalimu ni wajibu wa kisheria.
Kadhalika, katika hadithi ya Imam Sadiq (as):
«مَنْ أَصْبَحَ وَلَا یَهْتَمُّ بِأُمُورِ الْمُسْلِمِینَ فَلَیْسَ بِمُسْلِمٍ»"Mwenye kuamka asubuhi na hajali mambo ya Waislamu, basi si Mwislamu."
(al-Kafi, Juz. 2, uk. 164)
Kwa hivyo, dhulma ni sharti linalohitajika kwa ajili ya kudhihiri, lakini jukumu la kuiondoa liko juu ya waumini, kudhihiri kunatokea katika kilele cha dhulma, lakini hili halimaanishi kuhimiza dhulma; bali linaonyesha uhakika wa kutimia kwa uadilifu licha ya hali mbaya, mwenendo wa Imam Khomeini (r.a) katika kuanzisha serikali ya Kiislamu pia inachukuliwa kama kuandaa mazingira ya kudhihiri.
Hitimisho:
Dhulma ni mazingira yanayoandaa kudhihiri, si sababu ya moja kwa moja,
Kupambana na dhulma ni miongoni mwa vielelezo vya kusubiri faraj, na ukimya ni haramu.
Kuimarisha taasisi zinazodai uadilifu (hata kwa uwezo mdogo) ni wajibu wa kisheria.
Kwa mujibu wa maneno ya "Shahidi Sadr":"Kusubiri ni kiini cha uamsho, si lulu ya usingizi."
Kila hatua dhidi ya dhulma ni hatua kuelekea kudhihiri.
Maoni yako